Museveni awaonyesha Wabunge wa NRM ueledi wa ulengaji shabaha

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais Yoweri Kaguta Museveni  wa Uganda jana alikamilisha ziara ya Wabunge kwa kuwaonyesha mbinu za ulengaji shabaha katika taasisi ya kitaifa ya uongozi (NALI) wilayani Kyankwanzi.

Museveni aliwataka Wabunge hao kuwa mstari wa mbele kuwa na nidhamu na kukabiliana na rushwa.

Ziara hiyo ya siku tisa  ya Wabunge wa chama tawala cha National Resistance Movement (NRM) ilianza tarehe 7 mwezi huu.

Kwnye ziara hiyo Museveni aliwatembeza Wabunge shambani mwake eneo la Ngoma Wilayani Nakaseke na kuwaandalia sherehe kando na kuwaonyesha ng’ombe wake.

Aidha,Museveni aliahidi kuwatuza wambunge hao 359 shilingi milioni 3.5 za Kenya kila mmoja sawia na shilingi za Uganda milioni 100 punde watakapoapishwa mwezi ujao.

Share This Article