EPRA yapunguza bei ya mafuta ya Petroli na Dizeli

Dismas Otuke
1 Min Read

Mamlaka ya kudhibiti bidhaa za Petroli na kawi nchini (EPRA) Jumatano usiku imetangaza kupunguza bei za mafuta ya Petroli na Dizeli.

Hii ilifuatia hatua ya serikali kupunguza ushuru wa thamani ya bidhaa (VAT),kutoka asilimia 16 hadi asilimia 8.

Kulingana na bei zilizotangazwa Petroli ilipunguzwa kwa shilingi 9 na senti 37, huku bei mpya ikiwa shilingi 197.60, kwa lita moja.

Mafuta ya Dizeli yalipunguzwa kwa shilingi 10 na senti 21, na yatauzwa kwa shilingi 196.63, kwa kila Lita moja kuanzia leo Alhamisi Aprili 16.

Bei hiyo ilipunguzwa siku moja tu baada ya kupanda.

Wenye magari ya usafiri wa umma walitangaza kuongeza nauli jana siku moja tu baada ya bei mpya kutangazwa na EPRA.

TAGGED:
Share This Article