Klabu ya Kenya Pipeline(KPC) imeanza kwa ushindi mashindano ya klabu bingwa Afrika kwa wanawake baada ya kuilaza Kaubi Sporting Club(KSC) ya Ghana setio 3-0 katika mchuano wa ufunguzi wa kundi B Jumatatu alasiri nchini Misri.
KPC walitawala mechi hiyo wakisajili ushindi wa seti 3-0 za 25-19, 25-21, na 25-13.
Waakilishi hao wa Kenya wamejumuishwa kundi hilo ni LA LOI ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Gender Light ya Burkina Faso.
DCI pia ya Kenya inayoshiriki mashindano hayo kwa mara ya kwanza imerushwa kundi C pamoja na CF Carthage ya Tunisia,Nigeria Customs Service,,Kampala Capital City Authority ya Uganda na Eagles ya Congo.
Kenya Comercial Bank wamo kundi D hali kadhalika na Letto ya Cameroon,Vipers Partners kutoka Nigeria na Arsu ya Ushelisheli zimo kundi D.