Kinara wa Mawaziri Musalia Mudavadi siku ya Jumatatu amefanya mazungumzo na Balozi wa shirika la Umoja wa mataifa kuhusu mazingira (NEP),Mama Ida Odinga kwenye afisi yake jijini Nairobi.
Wawili hao walijadiliana kwa kina kuhusu jinsi ya kuboresha ushirikiano wa Kenya na UNEP.
Aidha, Mudavadi alimpongeza Ida kufuatia kuteuliwa kwakwe akiongeza kuhwa uongozi wake ni muhumu kwa Kenya kuendeleza ajenda kuhusu sera za mazingira.
Ulikuwa mkutano wa kwanza rasmi kati ya Mudavadi na mama Ida tangu ateuliw kuwa Balozi.