Junior Starlets waiparuza Nambia 2-1 ugenini

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya Kenya ya wasichana wasiozidi umri wa miaka 17 imesajili ushindi wa magoli 2-1  dhidi ya Namibia,katika mchujo wa kwanza kufuzu kwa fainali za Komeb la Dunia nchini Morocco.

Junior Starlets chini ya ukufunzi wa Midred Cheche, walianza mechi hiyo vyema huku wakichukua uongozi mapema kupitia kwa Lindey Atieno, kabla ya Faith Boke, kuongeza la pili na kuongoza 2-0 mwishoni mwa kipindi cha kwanza.

Wenyeji walikomboa bao moja mwishoni mwa kipindi cha pili.

Kenya wataialika Namibia wikendi ijayo kwa mchuano wa marudio huku mshindi akifuzu kwa raundi ya pili ambapo atamenyana na mshindi baina ya Uganda na Zimbabwe.

Share This Article