Washukiwa watatu wa uhalifu wakamatwa Meru

Tom Mathinji
1 Min Read
Washukiwa watatu wa uhalifu wakamatwa Laare, Meru.

Maafisa wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), wamewakamata washukiwa watatu wa uhalifu katika eneo la Laare, kaunti ya Meru.

Kwenye operesheni hiyo iliyotekelezwa baada ya maafisa hao kupashwa habari za kijasusi, bastola iliyokuwa na risasi nne pia ilipatikana.

Washukiwa hao James Chege, Mitiliano Muriuki, na Lawrence Mwilaria wanahusishwa na visa vya wizi katika eneo la Igembe na hivyo kusambaratisha usalama eneo hilo.

“Wakati wa kufanya upekuzi katika nyumba ya washukiwa hao, maafisa walipata bastola aina ya  Beretta 1934 Corto ikiwa na risasi nne,” ilisema DCI kupitia ukurasa wa X.

Kulingana na DCI, washukiwa hao wanazuiliwa huku maafisa wa polisi wakiendelea na uchunguzi.

TAGGED:
Share This Article