Gavana wa Benki kuu ya Kenya Dkt. Kamau Thugge amesema kuwa viwango vya riba vya asilimia 8.75 vimedumishwa, kwa lengo la kukabiliana na kupanda kwa gharama ya maisha hapa nchini.
Kulingana na Dkt. Thugge, Benki Kuu inajitahidi kuhakikisha viwango dhabiti vya vya ubadilishanaji wa pesa za kigeni na kupunguza bei za vyakula kutokana na mazingira bora yanayoshuhudiwa.
Kenya pia imefanyia marekebisho tathmini yake ya ukuaji wa uchumi ya mwaka huu kutoka asilimia 5.5 hadi asilimia 5.3 kwasababu ya gharama ya juu ya kawi ambayo itatatiza sekta ya utayarishaji bidhaa, uchukuzi, biashara na hoteli.
Dr Thugge alidokeza kuwa hali ya uchumi duniani inayumba huku gharama ya maisha ikitarajiwa kupanda kwasababu ya gharama ya juu ya kawi na na mbolea kutokana na vita vya mashariki ya kati.