Maafisa kutoka mamlaka ya kudhibiti bidhaa za petroli na kawi nchini (EPRA), wameendesha ukaguzi wa ghafla katika baadhi ya vituo vya mafuta nchini kuhakikisha vinaafiki viwango vinavyohitajika.
Kulingana na ukaguzi ulioendeshwa na maafisa wa EPRA ulibaini kuwa vingi vya vituo vya mafuta vimezingatia viwango vya ubora vilivyowekwa.
Aidha, EPRA wanafanya ukaguzi katika vituo hivyo kuhakikisha mafuta yanauzwa kwa bei zilizopendekezwa .
Watakaopatikana wamekiuka masharti yaliyowekwa na EPRA watatozwa faini isiyopungua shilingi milioni 10 au kifungo cha miaka mitano au zaidi au hukumu zote mbili.