Maafisa wa ujasusi wamelaani vikali kushambuliwa kwa Seneta wa Vihiga Godfrey Osotsi, hapo jana katika mkahawa Java katika jumaba la West End Mall, kaunti ya Kisumu.
DCI imesikistishwa na kitendo hicho cha kinyama ikiongeza kuwa inafanya uchunguzi kwa usaidizi wa video za CCTV za jumba hilo.
Hata hivyo Polisi wametaka umma kukoma kueneza uvumi na kupisha uchunguzi kufanyika .
Aidha, DCI imekariri kujitolea kupata chimbuko la shambulizi hilo na kuwakamata na kuwaadhibu kisheria wote waliohusika.
Osotsi alishambuliwa na kujeruhiwa na kundi la vijana ambao hawajatambulika na kujeruhiwa jana na yuko hospitalini akipokea matibabu.