Vituo vingi vya kuuza mafuta katika maeneo ya mashambani humu nchini jana vimeripoti upungufu mkubwa wa bidhaa hiyo muhimu.
Hatua hiyo yamkini ilisababishwa na upungufu wa mafuta yaliyosambazwa katika maeneo ya mashinani.
Foleni ndefu zilishuhudiwa huku baadhi ya vituo vikifunga kwa kukosa mafuta ya Petroli na Dizeli.
Maeneo ya mlima Kenya,Tranz Nzoia,Eldoret na katika vituo vilivyo mashinani bidhaa hiyo iliadimika huku vingine vikifanya kazi kwa kiwango chini ya asilimia 40.
Haya yanajiri licha ya serikali kutoa hakikisho la kuwepo kwa akiba ya kutosha ya mafuta humu nchini.
Hata hivyo vituo vya mafuta katika kaunti ya Nairobi na miji mingine mikuu humu nchini vilikuwa na mafuta ya kutosha na kutoshuhudia misongamano.