Mtandao wa kutuma maombi kwa kozi za masomo ya vyuo humu nchini (KUCCPS), umefunguliwa tena.
Katika kipindi cha mwezi mmoja ujao wanafunzi wanaotaka kujiunga na vyuo vya masomo ya kiufundi- TVET, watachagua kozi zao.
Wanafunzi wanaohitajika kutuma maombi ni wale waliokalia mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne- KCSE, mwaka 2025.