Mshukiwa wa uhalifu wa mtandaoni akamatwa Igembe Kaskazini

Tom Mathinji
1 Min Read

Maafisa wa polisi wamemkamata mshukiwa wa uhalifu wa mtandaoni katika kaunti ndogo ya Igembe Kaskazini.

Mshukiwa huyo alikamatwa baada ya Polisi kupashwa habari na wananchi kuhusu mienendo yake ya kutiliwa shaka.

Morris Kithinji Tirimiti, alitiwa nguvuni Jumanne jioni akiwa kwenye maficho yake katika eneo la Irindii, Laare, Igembe kaskazini.

Kulingana na Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai DCI, msako uliotekelezwa wakati mshukiwa huyo alipokamatwa, ulifanikisha kupatikana kwa simu sita za rununu zinazoaminika zimetumika kwenye shughuli za ulaghai.

Kadi 39 za simu pia zilipatikana, ishara kwamba mshukiwa huyo anahusika na mfumo mpana wa ulaghai.

Aidha DCI ilithibitisha kuwa mshukiwa huyo ana historia ya uhalifu na amewahi tumikia kifungo cha miaka 12 gerezani katika gereza la Naivasha.

Share This Article