Mchekeshaji na mwigizaji wa Uganda Anne Kansiime amefichua kwamba alijitolea mahari suala ambalo limeshangaza wengi wa wafuasi wake.
Alikuwa akizungumza kwenye mahojiano ambapo alisema kwamba alifanya mambo kama kawaida ambapo alipeleka mpenzi wake kwa wazazi, wakamkubali wakawa wanatarajia mahari.
Msanii huyo anasema wazazi waliitisha mahari muda mrefu, mume huyo hakutoa au kuonyesha nia ya, hadi Kansiime akaamua kujitolea mwenyewe.
“Nilijitolea mahari na nikashawishi ulimwengu na mume mwenyewe kwamba tumeoana,” alisema Kansiime huku akisisitiza kwamba yeye hajawahi kuwa mke.
Wanasema waliendelea na maisha yao kama kawaida huku wakisahau suala zima la mahari na yalivyotolewa lakini uongo huo uliokuwa na msingi hafifu ulisheheni kwa muda lakini ulifikia mwisho.
Msanii huyo anasema kwa sasa yeye na aliyekuwa mume wake Skylanta wanasaidiana kulea mwanao. Skylanta ambaye ni msanii alihama kutoka Mbarara na sasa anaishi karibu na shule ya mwanao.
Kansiime alimsifia Skylanta akisema kwamba anafurahia uhusiano alionao na mwanao.