ODPP yaimarisha vita dhidi ya ufadhili wa ugaidi

Viongozi wa mashtaka ya umma kutoka pembe zote za nchi, walishiriki mafunzo ya wiki moja kuhusu kutambua ufadhili wa ugaidi, uchunguzi na mbinu bora za kuendesha mashtaka mahakamani.

Tom Mathinji
1 Min Read
ODPP yaimarisha vita dhidi ya ufadhili wa ugaidi.

Afisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya umma (ODPP), inajizatiti kuimarisha vita dhidi ya ufadhili wa ugaidi, kwa kuhakikisha viongozi wa mashtaka ya umma wanapata ujuzi mwafaka.

Viongozi hao wa mashtaka ya umma kutoka pembe zote za nchi, walishiriki mafunzo ya wiki moja kuhusu kutambua ufadhili wa ugaidi, uchunguzi na mbinu bora za kuendesha mashtaka mahakamani.

Kupitia ukurasa wa X, afisi hiyo ilisema juhudi hizo ni sehemu yake ya mkakati mpana wa kuwawezesha maafisa wake kukabiliana na maswala ibuka ikiwa ni pamoja na uhalifu wa kiuchumi unaohusishwa na ugaidi.

“Mafunzo hayo yalijumuisha kutambua shughuli za ufadhili wa ugaidi, dalili za ufadhili huo, ukusanyaji wa ushahidi na kuwawezesha viongozi wa mashtaka kugundua mifumo tofauti ya malipo,” ilisema taarifa hiyo ya ODPP.

Washiriki walifahamishwa zaidi kuhusu mkakati wa kitaifa kuhusu athari za ufadhili wa ugaidi, unaowawezesha kuelewa zaidi hatari na mienendo tofauti ya ufadhili wa ugaidi hapa nchini.

TAGGED:
Share This Article