NTSA yaimarisha msako dhidi ya madereva wanaokiuka sheria barabarani

Dismas Otuke
1 Min Read

Mamlaka  ya Kitaifa ya Uchukuzi na Usalama Barabarani (NTSA) imekita kizuizi barabarani katika eneo la Uthiru kwenye barabara kuu ya Nairobi -Nakuru ili kukabiliana na madereva wanaokiuka sheria.

Mtego huo unawalenga madereva wanaorejea jijini Nairobi  na abiria baada ya sherehe za Sikukuu ya Pasaka.

Hatua hiyo inalenga kupunguza ajali za barabarani huku Wakenya wengi waliosafiri kuelekea mashinani wakirejea jijini Nairobi.

Ajali za barabarani zimekuwa tukio la kawaida nchini na kusababisha maafa ya watu wengi.

Siku chache zilizopita, watu 16 walifariki kwenye barabara kuu ya Nyeri-Nyahururu huku wengine kadhaa wakiuguza majeraha.

Ajali hiyo ilitokea katika eneo la Yunis na ilihusisha gari la kubeba abiria na lori.

Madereva wametakiwa kuwa waangalifu barabarani ili kuepusha maafa zaidi huku wito ukitolewa kwa wale wanaozembea kuchukuliwa hatua kali.

 

Share This Article