Bunduki 26 zasalimishwa Turkana

Dismas Otuke
1 Min Read

Bunduki 26 zilizokuwa zikimilikiwa kinyume cha sheria zimesalimishwa kwa maafisa wa polisi katika kaunti ya Turkana. 

Usalimishaji huo ni sehemu ya juhudi zinazoendelea za kuleta amani katika kaunti hiyo.

Polisi wamesema bunduki zilizosalimishwa ni pamoja na 21 za  AK-47, mbili za  M16, mbili za MK4 na moja ya G3 .

Hatua hiyo ni ufanisi mkubwa kwa serikali wa kurejesha amani katika eneo hilo la kaskazini mwa nchi ambalo limeghubikwa na wizi wa mifugo kwa muda mrefu.

Serikali imesema itafanya kila iwezalo kuwaangamiza majangili ambao wamekuwa wakiendeleza wizi wa mifugo na kuchangia ukosefu wa usalama katika eneo hilo.

TAGGED:
Share This Article