Msanii wa muziki nchini Tanzania Rosary Robert Iwole maarufu kama Rosa Ree amemuaga babake mpendwa Robert Iwole, aliyeaga dunia kwa majonzi mengi kupitia akaunti yake ya Instagram.
“Umenifundisha aina tofauti ya kuaga, ambayo sijui jinsi ya kusema…. Huenda haupo hapa, lakini najua haujaondoka. Imani iko sawa na roho yako, safiri salama Baba,” aliandika msanii huyo chini ya picha kadhaa alizochapisha za hafla ya mazishi ya mzee huyo.
Akizungumza kwenye mahojiano na kituo cha redio cha East Africa, Rosa alisema kwamba babake aliyefariki akiwa na umri wa miaka 72, hakuwa na matatizo ya kiafya bali aliugua muda mfupi na kufariki.
“Ameumwa kama wiki mbili zilizopita akawa amelazwa hospitali, baada ya siku chache akarudi nyumbani wakasema shindikizo la damu na cholesterol” alisema Rosa Ree.
Baada ya hapo Mzee Iwole alirejeshwa hospitalini alipozidiwa ambapo hakukaa sana na kisha akakata roho. Mwili wake ulipumzishwa kaburini nyumbani kwake mwezi uliopita.