Murkomen amtembelea Mkurugenzi wa halmashauri ya bandari nchini William Ruto

Dismas Otuke
0 Min Read

Waziri wa usalama wa kitaifa Kipchumba Murkomen amemtembelea Mkurugenzi wa halmashauri ya bandari nchini William Ruto,anayepokea matibabu katika hospitali moja ya Mombasa, baada ya kuhusika kwenye ajali ya barabarani Ijumaa usiku.

Ruto alimpoteza bintiye kwenye ajali hiyo   huku wanawe wengine wawili na mpwa wake wakinusurika na majeraha madogo.

Kulingana na Murkomen madaktari wametoa ahadi ya kuhakisha Mkurugenzi huyo wa bandari anapata afueni ya haraka na kuondoka hospitalini.

Share This Article