Afisa Mkuu Mtendaji wa KPA ajeruhiwa kwenye ajali ya barabarani

Tom Mathinji
1 Min Read
Afisa Mkuu Mtendaji wa KPA William Ruto.

Halmashauri ya Bandari Nchini (KPA), imetangaza kuwa Afisa Mkuu Mtendaji William Ruto, anapokea matibabu hospitalini baada ya kuhusika katika ajali ya barabarani Ijumaa jioni.

Kupitia kwa taarifa, halmashauri hiyo ilithibitisha kuwa mtoto wa kike wa Ruto alifariki kwenye ajali hiyo, huku jamaa kadhaa wa familia hiyo pia wakilazwa hospitalini.

“Tuna huzuni kutangaza kuwa Afisa Mkuu Mtendaji William K. Ruto, alihusika kwenye ajali ya barabarani Ijumaa jioni alipokuwa akisafiri na familia yake,” ilisema taarifa hiyo.

“La kusikitisha ni kwamba mtoto wake wa kike aliangamia katika ajali hiyo,” iliongeza taarifa hiyo.

Hata hivyo, KPA ilithibitisha kuwa Ruto yuko katika hali nzuri na wanapokea matibabu chini ya uangalizi wa karibu.

Aidha, KPA ilidokeza kuwa inashirikiana na asasi husika kuchunguza chanzo cha ajali hiyo.

“Tunawatakia uponyaji wa haraka,” iliongeza KPA.

Share This Article