Wakristo wahimizwa kuonyesha upendo wakati huu wa Pasaka

Tom Mathinji
1 Min Read
Naibu Rais Prof. Kithure kindiki.

Huku Wakristo wanapojiunga na ulimwengu kuadhimisha Siku Kuu ya Pasaka, Wakenya wamehimizwa kuchukua msimu huu kutafakari, kuwa na mwanzo mpya na kuonyesha upendo.

Kwenye ujumbe wake kwa taifa, Naibu Rais Prof. Kithure Kindiki alisema kifo cha Yesu Kristo ni dhihirisho kuu la upendo, akidokeza kuwa imani yetu hufanywa upya wakati wa kipindi hiki cha pasaka.

Naibu Rais alibainisha kuwa Pasaka inatoa fursa ya matumaini na ukombozi, akiongeza kuwa ni ishara ya wakati maalum katika safari ya kiroho ya waumini.

“Tunatakia kila familia amani. Taifa letu lifanyekazi kwa pamoja ili kuafikia malengo yake,” alisema naibu huyo wa Rais.

Naibu Rais aliitaja wikendi ya Pasaka kuwa kipindi muhimu cha kutafakari, na mwamko mpya, akitoa wito kwa wakenya kutafakari kwa kina maana ya Pasaka.

Kindiki pia alizitakia heri njema familia kote nchini, akielezea matumaini ya amani na umoja.

Share This Article