Maafisa wa polisi katika kaunti ya Kwale wamenasa misokoto 1,858 ya bangi katika kaunti ya Kwale katika juhudi za kukabiliana na ulanguzi wa mihadarati.
Polisi kutoka kituo cha Diani waliopewa vidokezo na umma walitekeleza msako katika kitongoji cha Mwakipeku, wadi ya Kinondo katika kaunti ndogo ya Msambweni na kupata misokoto hiyo na kumtia mbaroni mshukiwa mmoja.
Mshukiwa huyo yuko korokoroni akisubiri kufikishwa kortini.