Majeshi ya Israel yakiri kuwaangamiza wanamngambo 40 wa Hezbollah

Dismas Otuke
1 Min Read

Majeshi ya Isreal yamekiri kuwaua wanamgambo 40 wa kundi la Hezbollah katika kipindi cha saa 24 zilizopita.

Kulingana na taarifa hiyo majeshi ya Israel yalishambulia kutoka angani kambi za wanamgambo wa Hezbollah na maeneo ya kuhifadhi silaha.

Aidha, Israel ilitekeleza mashambulizi katika jela linalotumiwa na Hezbollah kusini mwa Lebanon, na pia kufanya mashambulizi mengine ya majini na nchi kavu na kuwaua wanachama 40 wa kundi hilo.

Wakati uo huo pia Hezbollah wamekiri kuzima mashambulizi kadhaa ya majeshi ya Israel na pia yameshambulia kwa roketi eneo la Metula nchini Israel.

Share This Article