Mamlaka ya Maadili na Kupambana na Ufisadi nchini, EACC, imewakamata watu wawili kwa kusingizia kuwa maafisa wa tume hiyo na kuwatapeli raia.
Washukiwa, Annastacia Mueni Kavemba na Stephen Muleu Ngati, walikamatawa kufuatia malalamishi yaliyowasilishwa kwenye tume hiyo Machi 29, 2026.

Kulingana na ripoti, Mueni aliwasiliana na mlalamishi na kujitambua kama afisa wa EACC. Alidai kuwa mlalamishi alikuwa akichunguzwa na kuitisha fedha kushawishi matokeo ya uchunguzi huo na kuzuia hatua zaidi kuchukuliwa dhidi ya mlalamishi.
Tume ilianzisha uchunguzi kufuatia malalamishi hayo na kusababisha kukamatwa kwa washukiwa punde baada ya kupokea hongo ya shilingi 20,000.
Washukiwa kwa sasa wapo katika makao makuu ya ACC kuandikisha taarifa wakisubiri kufikishwa mahakamani.