Mahakama siku ya Jumamosi iliidhinisha ushindi wa Rais Dennis Sassou Nguesso kuendelea kuliongoza taifa la Congo Brazzavile baada ya kuzoa ushindi wa takriban asilimia 95 katika uchaguzi mkuu wa tarehe 15 mwezi huu.
Nguesso aliye na umri wa miaka 82, ameanza kuhudumu katika wadhfa wa urais kwa kipindi cha tano cha miaka mitano.
Mahakama ilikiri kuwa Nguesso alipata ushindi wa asilimia 94.9 ya kura zote zilizopigwa huku asilimia 65.9 ya wapigaji kura ikijitokeza debeni.