Mudavadi ashinikiza mipango ya kukabiliana na mafuriko Nairobi

Tom Mathinji
1 Min Read

Mkuu wa Mawaziri Musalia Mudavadi, ametangaza juhudi kabambe za kukabiliana na mafuriko Jijini Nairobi,  akitoa wito wa mipango ya dharura ya kulinda maisha na mali.

Waziri huyo akidokeza kuwa ili kukabiliana na mafuriko Nairobi, ipo haja ya kuwa na suluhu za muda mrefu.

Aliyasema hayo aliposhiriki mazungumzo na ujumbe kutoka kampuni ya Maji na Majitaka ya Nairobi na Ile ya Dredge Masters kutoka Ghana, kukadiria hali ya bwawa la Nairobi na kuharakisha mipango ya kusafisha mito mitatu ya Nairobi.

“Lengo letu ni wazi, kudhibiti mapito ya maji na kuzuia kuzuka tena kwa mafuriko ambayo inahatarisha maisha na uharibifu wa Mali,” alisema Mudavadi.

Alidokeza kuwa mikakati hiyo haitaangazia tu na Nairobi, lakini itapanuliwa katika maeneo mengine ambayo hukumbwa na mafuriko.

Share This Article