Mahakama moja ya Kajiado, imemhukumu miaka 20 gerezani mshukiwa anayedaiwa kumdhulumu kimapenzi msichana wa umri wa miaka 12.
Msichana huyo inadaiw alidhulumiwa na mshukiwa huyo Oktoba 15, 2021, alipokuwa akiwahudumia wageni baada ya hafla ya mazishi.
Miongoni mwa wageni waliokuwa wakihudumiwa na msichana huyo ni mshukiwa ambaye alimhadaa atoke nje ishara kwamba anataka kumuuliza swali, lakini badala yake alianza kumdhulumu kimapenzi.
Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Mkuu wa mahakama hiyo Susan N. Mwangi, alisema upande wa mashtaka uliwasilisha ushahidi wa kutosha ikiwa ni pamoja na ripoti ya kimatibabu kuthibitisha mshukiwa huyo alitekeleza uhalifu huo.
Upande wa mashtaka ukiongozwa na Linda Nzioka, uliwasilisha mashahidi watano mahakamani, waliothibitisha mshukiwa huyo alitekeleza uhalifu huo.