Runinga ya kitaifa ya KBC Channel 1, itarusha mubashara mechi ya kimataifa ya kirafiki kati ya Kenya na Estonia leo kuanzia saa moja usiku kutoka uwanja wa Amahoro mjini Kigali, Rwanda.
Mechi hizo maarufu kama FIFA Series zinaleta pamoja mataifa manne katika kundi moja na Kenya, huku ikiwa mara ya kwanza kwa Harambee Stars kuchuana na Estonia.
Kenya ni ya 113 huku wapinzani wao wakishikilis nafasi ya 128 katika msimamo wa FIFA.
Wenyeji Rwanda watakumbana na Grenada katika mchuano wa pili kuanzia saa nne usiku katika uwanja uo huo.
Washindi wa leo watachuana kwenye fainali ya Jumatatu ijayo, ilhali watakaoshindwa watakabiliana kwenye mechi ya kutafuta mshindi wa nafasi ya tatu.