Timu ya taifa ya soka ya Kenya, Harambe Stars leo Ijumaa jioni itakuwa na kibarua kigumu itakapomenyana na Estonia katika mechi za kirafiki almaarufu FIFA Series katika uwanja wa Amahoro mjini Kigali, Rwanda.
Pambano hilo linatarajiwa kungóa nanga saa moja jioni huku mshindi akiweka miadi kuchuana kwenye fainali na atakayeshinda mechi nyingine kati ya wenyeji Rwanda Grenada.
Fainali itapigwa Jumatatu ijayo ikitanguliwa na mechi ya kutafuta mshindi wa tatu na nne kwa timu zitakazoshindwa leo.
Stars wamekuwa Kigali tangu mapema wiki hii kwa maandalizi ya mechi hizo mbili za kujinoa makali.