Wafanyabiashara wahaha kukamilisha matakwa ya KRA kabla ya mtandao kufungwa

Dismas Otuke
1 Min Read

Wafanyabiashara wengi wamo katika hekaheka za kukamilisha malipo na matakwa ya Mamlaka ya Mapato nchini (KRA ) kupitia kwa mtandao wa forodha wa iCMS kabla ya kufungwa kwa mtandao huo ili kukarabatiwa.

Mtandao wa KRA wa kulipia mizigo forodhani unatarajiwa kufungwa kati ya Aprili 4 hadi 6 mwaka huu.

Mtandao huo pia ulifungwa mwezi jana kwa zoezi sawia na hilo na kusababisha msongamano mkubwa katika Bandari ya Mombasa.

Wafanyabiashara hutumia mtandao wa iCMS kupata idhini kuchukua mizigo yao kutoka bandari ya Mombasa.

 

TAGGED:
Share This Article