Salah kuondoka Liverpool mwishoni mwa msimu huu

Martin Mwanje
1 Min Read
Mchezaji Mohamed Salah

Mshambulizi matata wa klabu ya Liverpool Mohamed Salah ametangaza kuwa ataigura klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu.

Awali, kulikuwa na uvumi kwamba angetalikiana na Anfield kabla ya kuanza kwa msimu huu kutokana na tofauti zilizoibuka kati yake na kocha Arne Slot.

Salah, anayetokea Misri, alijiunga na klabu hiyo mwaka 2017 na amekuwa nguzo muhimu kwa ufanisi wa timu hiyo tangu wakati huo.

Amesakata zaidi ya mechi 400, kutia kimiani magoli zaidi ya 250 na kushinda mataji kadhaa ikiwa ni pamoja na ligi kuu na UEFA.

Salah ametangaza dhamira yake ya kuihama Liverpool wakati ambapo timu hiyo inasuasua kwenye ligi kuu.

Mwishoni mwa juma lililopita, ilicharazwa magoli 2-1 na timu ya Brighton katika uwanja wa Amex.

Kwa sasa, vijana hao wa Arne Slot wanashikilia nafasi ya 5 kwa alama 49 kwenye jedwali la ligi kuu.

 

 

TAGGED:
Share This Article