Wito wa watoto walemavu kupata elimu watolewa Kilifi

radiotaifa
1 Min Read
Picha kwa hisani ya Soo TV

Taarifa ya Dickson Wekesa

Wazazi wa watoto walemavu wametakiwa kuhakikisha watoto hao wanahudhuria masomo shuleni na hawanyimwi huduma muhimu katika jamii.

Wito huo umetolewa na Naibu Kamishna wa eneo la Kilifi Kaskazini Samuel Mutisya aliyezungumza wakati wa mkutano wa washikadau wa kutetea haki za walemavu.

Mkutano huo uliandaliwa na shirika la Disability With Ability (DIWA) mjini Kilifi, kaunti ya Kilifi.

Mutisya alilamika kuwa wazazi wengi hasa katika maeneo ya mashinani bado wanawaficha watoto wao walemavu na kwa kufanya hivyo kuwanyima fursa mbalimbali maishani.

Alisema kuna haja ya kuwepo usawa na haki inapokuja kwa masuala ya fursa za ajira, utoaji zabuni serikalini na kushiriki siasa miongoni mwa masuala mbalimbali.

Kwa upande wake, Mkurgenzi wa DIWA Susan Kitheka alilalama kuwa idadi ya walemavu nchini ni kubwa ilhali mahitaji yao mara nyingi hupuuzwa.

Alisema kuna mapengo bayana yaliyopo kati ya ulemavu na sekta mbalimbali kama vile elimu, afya, ufadhili na biashara, hali ambayo alisema inapaswa kuangaziwa.

Angalau asilimia 15 ya watu wote nchini Kenya ni walemavu, hii ikiwa ni sawa na watu zaidi ya milioni 8.

TAGGED:
Share This Article