Viongozi Machakos wataka IEBC kukomesha hulka ya utoaji hongo

radiotaifa
1 Min Read
Erastus Ethekon - Mwenyekiti wa IEBC

Taarifa ya Jonathan Musau

Muungano wa viongozi wa makanisa eneo la Ukambani umeshtumu vikali Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini, IEBC kwa kushindwa kukomesha hulka ya viongozi wa kisiasa kutoa hongo kwa wapiga kura.

Viongozi hao walitoa shutuma hizo wakati wakiwahutubia wanahabari mjini Machakos.

Wakiongozwa na mwenyekiti wao askofu Timothy Ndambuki, walisema hongo imechangia pakubwa Wakenya kukosa kuchagua wanasiasa wenye maadili mema.

Wakati huohuo, Ndambuki ambaye pia ndiye askofu mkuu wa kanisa la ABC amewakosoa wapiga kura kwa kukosa kuzingatia sera wanapofanya maamuzi ya viongozi wanaowachagua.

Matamshi yake yanakuja wakati ambapo wanasiasa wameanza kuwarushia wapiga kura chambo kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.

Madai ya utoaji hongo huchacha wakati wa kampeni za kuelekea uchaguzi huo.

Share This Article