Nicki Minaj anashtakiwa mahakamani kwa madai ya kushindwa kulipa kampuni inayodai kwamba ilitoa zaidi ya dola elfu 275, kugharamia maandalizi na gharama nyingine kwa yake matamasha mawili.
Kulingana na nyaraka za mahakama kampuni iitwayo 24/7 Productions inamshtaki Nicki na kampuni yake iitwayo Pink Friday Productions.
24/7 inasema ilianza kufanya kazi na Nicki kwenye Tuzo za MTV Video Music Awards za mwaka 2022, ambapo ilitoa huduma za maandalizi ya burudani ya moja kwa moja.
Mwisho wa mwaka 2023, kampuni hiyo inasema Nicki aliwaomba wamsaidie na matamasha yake ya Jingle Ball na uzinduzi wa albamu yake “Pink Friday 2.”
Kampuni hiyo inadai iliwasilisha bajeti kwa timu ya Nicki — ambazo wanasema ziliidhinishwa — na pia ilitoa mipango ya awali, usimamizi wa moja kwa moja kwenye eneo la tukio, wafanyakazi, sauti, taa, miundombinu ya jukwaa, usafiri wa ardhini na uratibu wa jumla.
24/7 Productions inasema ilitoa zaidi ya dola 275,000 kwa niaba ya Nicki kwa ajili ya gharama hizo, fedha ambazo zilipaswa kulipwa baadaye.
Kampuni hiyo inadai kuwa kampuni ya Nicki ililipwa takriban dola 650,000 kwa onyesho lake la Jingle Ball pekee lakini haikuwahi kulipa deni la 24/7.
Kampuni hiyo inasema imejaribu kupata fedha hizo kwa miaka kadhaa, lakini inadai timu ya Nicki imekuwa ikijibu kwa kauli inayorudiwa mara kwa mara: “Tutalifuatilia suala hili.”
Sasa kampuni hiyo inamshtaki kwa kuvunja mkataba na madai mengine, na inadai fidia inayozidi dola 275,000 kutoka kwa Nicki.