Kenya kuimarisha ushirikiano na Indonesia katika sekta ya afya

Dismas Otuke
1 Min Read

Kenya inalenga kuimarisha ushirikiano na Indonesia katika juhudi zitakazoboresha sekta ya afya humu nchini.

Hii ni kwa mujibu wa Waziri wa Afya Aden Duale aliyezungumza alipompokea Balozi wa Indonesia humu nchini Witjaksono Adji aliyemtembelea afisini leo Jumatatu.

Mazungumzo baina ya wawili hao yalihusu ubunifu katika sekta ya afya, famasia, nguvukazi na teknolojia ya kisasa katika afya.

Mkutano huo pia ulihudhuriwa na Katibu wa Afya ya Umma bi Mary Muthoni na Mkurugenzi Mshirikishi wa Sekta ya Afya Dkt. Omar Ahmed.

Share This Article