Taarifa ya Jonathan Musau
Baraza Kuu la Maimamu na Wahubiri wa humu nchini, CIPK limepongeza Wakenya walioonyesha ukarimu kwa waumini wa dini ya Kiislamu katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Mwenyekiti wa baraza hilo eneo la Lower Eastern Sheikh Anas Abdalah anasema ukarimu huo ulisaidia Waislamu kufanikisha mfungo wao.
Amesema haya mapema leo Ijumaa katika msikiti wa Jumia mjini Machakos.
Hii ni baada ya kuongoza swala maalum ya sikukuu ya IDD ambapo pia amewapongeza wafanyabiashara walioamua kupunguza bei ya bidhaa mbalimbali hasa zinazotumika sana na Waislamu wakati wa Ramadhani.