Shirika la ndege la Kenya Airways (KQ) na lile la CemAir la Afrika Kusini, yametia saini Mkataba wa Maelewano kuimarisha uchukuzi wa angani barani Afrika.
Kupitia kwa taarifa leo Alhamisi kwenye ukurasa wa X, shirikala KQ lilisema ushirikiano huo utapanua ufikiaji wa masoko muhimu katika maeneo ya Kusini, Mashariki na Magharibi mwa Afrika.
“Ushirikiano huu, utawezesha kufika maeneo ya Bloemfontein, Hoedspruit na George nchini Afrika Kusini pamoja na Victoria Falls, Maun na Harare, huku miji kama vile Zanzibar, Accra Kigali kupitia Nairobi ikipanuka,” ilisema taarifa hiyo ya KQ.
Aidha shirika hilo la ndege lilidokeza kuwa ushirikiano huo utafanikisha usafiri usio na matatizo kupitia utangamano ulioimarishwa wa wateja.
“Pamoja tunaendelea kuunganisha watu wa Afrika, tamaduni zao na masoko pamoja na kutoa fursa mpya katika bara Afrika.