Mshukiwa wa ulaghai afikishwa mahakani Kirinyaga

Tom Mathinji
1 Min Read
Mshukiwa wa ulaghai afikishwa mahakamani Kirinyaga.

Mshukiwa wa ulaghai amefikishwa mahakamni baada ya kuwalaghai wananchi shilingi 3,000,000 kwa madai kwamba angeweza kuwasaidia kujiunga na Huduma ya Taifa ya Polisi.

Hatua hiyo ni baada ya wananchi watatu kuripoti kisa hicho katika kituo cha polisi cha  Wang’uru, waliodai kuwa mshukiwa huyo  Mercy Prudence Mbaika Mutie, aliwahadaa kwamba angeweza kuwasaidia waajiriwe katika Huduma ya Taifa ya Polisi.

Kupitia ukurasa wa X, Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), ilisema kuwa waathiriwa hao walimkabidhi pesa mshukiwa huyo ili afanikishe ajira yao.

Hata hivyo baada ya kupokea fedha hizo, mshukiwa huyo alienda mafichoni.

Baada ya uchunguzi wa kina, maafisa wa DCI kutoka Mwea Mashariki, mshukiwa huyo alisakwa na kukamatwa ambapo alifikishwa matika Mahakama ya  Wang’uru.

Alishtakiwa kwa kupokea fedha kwa njia ya udanganyifu na aliachiliwa kwa dhamana ya shilingi 500,000.

Share This Article