Idadi ya walioangamia kwa mafuriko nchini yafikia 66

Dismas Otuke
1 Min Read

Huduma ya Kitaifa ya Polisi, NPS, imesema kuwa idadi ya watu waliofariki kutokana na mafuriko nchini imefikia 66.

Idadi hiyo inajumuisha wanaume 50, wanawake wanane na watoto wanane.

Kaunti ya Nairobi ndiyo iliyokuwa na maafa mengi ikiwa na vifo 33, ikifuatwa na eneo la Mashariki kwa vifo 18 huku watu wanane kutoka Bonde la Ufa wakiripotiwa kuangamia.

Aidha, polisi wameongeza kuwa zaidi ya familia 2,000 zililazimika kuhama makwao kutokana na mafuriko.

 

TAGGED:
Share This Article