Kiongozi Mkuu mpya wa Iran Mojtaba Khamenei ameapa kulipiza kisasi dhidi ya Marekani na Israel.
Nchi hizo mbili zimekuwa zikifanya mashambulizi makali mjini Tehran.
Hii ni mara ya kwanza kwa Khamenei kutoa taarifa tangu alipochukua usukani kama Kiongozi Mkuu wa Iran.
Taarifa yake ilisomwa kwenye runinga ya serikali jana Alhamisi.
Inatoa wito wa umoja wa kitaifa na kuwataka raia wa taifa hilo kuendelea na mapigano.
Inaongeza kuwa Marekani sharti ifunge kambi zake za kijeshi zilizopo kanda hiyo la sivyo ikabiliwe kwa mashambulizi.
Jana Alhamisi, Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu kilisema kimeshambulia meli ya mafuta inayomilikiwa na Marekani baada ya wafanyakazi wake kupuuza maonyo yake. Meli hiyo ilikuwa ikipeperusha bendera ya Visiwa vya Marshall katika Ghuba ya Uajemi.
Khamenei pia amesema Mlango Bahari wa Hormuz utaendelea kufungwa ili kumshinikiza adui.