Serikali yahimizwa kuwezesha vyuo vya TVET

radiotaifa
1 Min Read

Taarifa ya Jonathan Musau

Serikali imehimizwa kuwezesha taasisi za kiufundi, TVET za kibinafsi kama mbinu mojawapo ya kukabiliana na changamoto ya ajira miongoni mwa vijana nchini.

Afisa Msimamizi wa Taasisi ya Mafunzo ya Mutisya mjini Machakos Julius Mutua Mwamisi anasema endapo serikali itapiga jeki kifedha taasisi hizo, basi hatua hiyo itaziwezesha kupunguza karo.

Kulingana naye, upunguzaji huo utachangia kuongezeka kwa wanafunzi wanaojiunga na taasisi za TVET nchini.

Mwamisi amesifia elimu ya vyuo vya TVET akisema baada ya kufuzu, mmoja anapata maarifa ya kujiajiri na hivyo kupunguza idadi ya vijana wasio na ajira nchini.

Share This Article