Mahusiano ya jinsia moja kuadhibiwa vikali nchini Senegal

Dismas Otuke
0 Min Read

Watakopatikana na hatia ya kushiriki mahusiano ya jinsia moja nchini Senegal watapokea adhabu kali.

Hii ni baada ya bunge kupitisha sheria kali zilizoongeza maradufu adhabu ya awali kwa kosa hilo.

Sheria hiyo ilipata uungwaji mkono kutoka kwa wabunge 135 na hakuna aliyeipinga.

Watakaopatikana na kosa la kushiriki mahusiano ya jinsia moja watahukumiwa kifungo cha miaka 10 gerezani na kutozwa faini ya shilingi milioni 1.4 za Kenya.

TAGGED:
Share This Article