Putin ampongeza kiongozi mpya wa Iran

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais wa Russia Vladmir Putin.

Rais wa Russia Vladimir Putin, amempongeza rais mpya wa Iran Mojtaba Khamenei, kufuatia kucteuliwa kwake kuwa kiongozi mkuu wa nchi hiyo.

Kulingana na taarifa kutoka Russia, Putin  alimpongeza Mojtaba Khamenei baada ya kumtumia ujumbe kupitia telegram siku ya Jumatatu.

“Huku Iran inapokabiliana na mashambulizi, unahitaji ujasiri wa hali ya juu unapotekeleza majukumu yako. Nina imani kuwa utaendeleza kazi ya baba yako na kuwaunganisha raia wa Iran,” ilisema taarifa kutoka Kremlin.

Kulingana na taarifa hiyo, Putin alieleza kuunga mkono Iran, akidokeza kuwa Iran itaendelea kuwa mshirika wake wa kutegemewa.

“Ningependa kuthibitisha uungaji mkono wangu wa Tehran. Russia imekuwa na itaendelea kuwa mshirika wa kutegemewa wa Jamhuri hiyo ya Kiislamu. Nakutakia ufanisi unapotatua jukumu ngumu mbele yako, pia nakutakia afya njema na nguvu zaidi,” iliongeza taarifa hiyo.

Mojtaba Khamenei, mwenye umri wa miaka 56,ndiye kiongozi mkuu wa tatu wa Iran katika historia ya taifa hilo.

Rais wa Iran Masoud Pezeshkian alitaja uteuzi wake kuwa hatua kubwa katika kuimarisha umoja wa nchi hiyo.

Share This Article