Wabunge wamepinga pendekezo la kuongeza pesa za ukarabati wa afisi ya Mkuu wa Mawaziri Musalia Mudavadi kwa shilingi bilioni moja zaidi.
Haya yanajiri siku chache baada ya kuibuka kwa madai kwamba bajeti ya ukarabati wa Ikulu ya Rais tayari imeongezeka maradufu kutoka kwa kiwango cha awali.
Mudavadi amekuwa akipigania kuongezewa bajeti ya ukarabati wa afisi yake ya kupangisha katika makao makuu ya Railways, kaunti ya Nairobi.
Wabunge walikuwa wamepokea pendekezo la kuidhinisha shilingi bilioni moja za ukarabati wa afisi ya Mudavadi.