Aliyekuwa mkufunzi wa zamani wa timu ya taifa ya soka, Harambee Stars Engine Firat, amefariki dunia mapema Jumatatu akiwa na umri wa miaka 55.
Yamkini, raia huyo wa Uturuki alianguka na kuzirai akiwa katika uwanja wa ndege wa Istanbul baada ya kupatwa na mshtuko wa moyo akiwa safarini kutoka Beirut kuelekea Adana muda mfupi baada ya kutoka mjini Lebanon.
Hadi kifo chake, Firat alikuwa kocha wa klabu ya Nejmeh SC na aliwaongoza kwa mara ya mwisho tarehe 9 mwezi uliopita.
Klabu ya Nijmeh inachezewa na Wakenya Austin Odhiambo, Anthony Akumu, na Masoud Juma.
Aliongoza Harambee Stars hadi mwaka 2024, kabla ya kufanya kazi katika mataifa ya
Moldova, ana Iran, kabla ya kutua ebanon.
Rais wa Shirikisho la Soka la Humu Nchini Hussein Mohammed ametuma risala za rambirambi kufuatia kifo hicho.