Idara ya GSU imeshirikiana na tawi la FKF Nairobi West kuandaa mechi za kirafiki kama njia ya kukuza soka mashinani na kuboresha ushirikiano baina ya maafisa wa polisi na jamii.
Kulingana na ushirikiano huo, GSU wataandaa mechi kadhaa za kirafiki katika mitaa ya mabanda katika kaunti ya Nairobi ili kuhamasisha umma kuhusu umuhimu wa ushirikiano baina ya polisi na jamii katika kuleta amani.
Wazee wa GSU walitoka sare ya bao moja kwa moja dhidi ya wazee wa Dagoreti katika mechi ya wanaume huku wasichana wa City Inspectorate wakiwalemea Vipawa Ladies bao moja kwa bila.
Awali wachezaji wat imu ya Red Berets kutoka GSU inayoshiriki ligi ya divisheni ya kwanza ya FKF walizuru makao ya watoto cha Real Hope mtaani Kawangware na kutoa msaada wa vyakula na vifaa vya usafi.