Baadhi ya Marais wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), leo Jumamosi walishiriki Mkutano wa Faragha kabla ya kuanza kwa Mkutano wa 25 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi.
Marais waliohudhuria mkutano huo wa faragha ni pamoja na Dkt. Samia Suluhu Hassan (Tanzania), Rais wa Kenya ambaye pia ni Mwenyekiti wa sasa wa EAC, Dkt. William Ruto, Yoweri Museveni (Uganda), Hassan Sheikh Mohamud (Somalia) na Rais wa Burundi, Évariste Ndayishimiye.
Kwenye mkutano huo, Rwanda inawakilishwa na Waziri Mkuu Dkt. Justin Nsengiyumva huku Sudan Kusini ikiwakilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje Semaya Kumba.
Mkutano unafanyika leo Jumamosi katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC), mkoani Arusha.
Kauli mbiu ya mkutano huo ni “Kuimarisha utangamano ili kuboresha maisha ya raia wa Afrika Mashariki,”.