Rais Willing Ruto Leo Jumamosi amewasili Jijini Arusha Tanzania, kuhudhuria mkutano wa 25 wa viongozi wa jumuiya ya Afrika Mashariki.
Kulingana na Rais Ruto, mkutano huo unalenga kuimarisha utangamano wa kikanda, ushirikiano wa kiuchumi na kuunganisha raia wa Kanda hiyo.
Mkutano huo pia unahudhuriwa na Mawaziri, Maafisa Wakuu serikalini, viongozi wa mashirika ya kimataifa, wataalam wa kiuchumi wa Kanda, washirika wa maendeleo, viongozi wa biashara na wale wa kijamij.
Marais wengine wanaohudhuria mkutano huo ni pamoja na Samia Suluhu Hassan wa Tanzania, Yoweri Museveni (Uganda), Paul Kagame (Rwanda), Erariste Ndashimiye (Burundi), Salva Kiir Sudan Kusini), Felix Tshisekedi (DRC), na Hassan Sheikh Mohamud (Somalia).
Kauli mbiu ya mkutano huo ni “Kuimarisha utangamano ili kuboresha maisha ya raia wa EAC”.