Safaricom: Idadi ya wateja wa M-PESA imefika milioni 40

radiotaifa
1 Min Read
Wateja wa M-PESA wafika milioni 40, imesema Safaricom.

Kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi Safaricom, leo Ijumaa imetangaza kwamba idadi ya wateja wa M-PESA imefikia milioni 40, huku inaposherehekea miaka 19 ya ujumuishaji wa kifedha.

Kwenye taarifa kampuni hiyo imesema kuwa tangu mfumo wa M-PESA ulipozinduliwa tarehe 6 mwezi Machi mwaka 2007, umeimarika kutoka uhamishaji pesa baina ya watu na kuwa mshirika wa kifedha katika maisha ya kila siku.

Ilisema kuwa mfumo huo ulioanza kama mbinu ya kutuma pesa umeimarika na kujumuisha uwekezaji na usimamizi  wa mali kupitia mpango wa hazina ya soko la fedha wa Ziidi MMF, mfumo wa biashara wa Ziidi, huduma za mikopo zikiwemo Fuliza na KCB M-PESA, na suluhu za kibiashara zikiwemo Lipa na M-PESA, Pochi la Biashara na Global Pay.

Mpango huo pia umeondoa vikwazo katika kupata fursa za kuleta utajiri na hivyo kuwafanya wakenya zaidi kupanga, kuweka akiba na kuwekeza.

Share This Article