Aliyekuwa Gavana wa Kiambu Ferdinand Waititu, aliachiliwa huru siku ya Alhamisi kutoka korokoroni na Mahakama Kuu akisubiri uamuzi wa rufaa ya kesi inayomkabili ya wizi wa shilingi milioni 588 za ujenzi wa barabara za kaunti.
Uamuzi wa jana ulikuwa afueni kwa Waititu ambaye amekuwa akitumikia kifungo kwenye gereza la Kamiti Maximum, tangu alipohukumiwa Februari mwaka uliopita.
Katika kesi hiyo, Waititu anakabiliwa na mashtaka ya kutoa kiholela zabuni za shilingi milioni 588 za ujenzi wa barabara za kaunti.
Jaji Wilfrida Okwany alikubali ombi la wakili wa Waititu, aliyetaka dhamana yake ipunguzwe kutoka shilingi milioni 53 hadi milioni 20 na mdhamini wa kiwango sawa cha pesa.
Kesi hiyo itatajwa tena tarehe 14 mwezi ujao.