Maafisa wa polisi wamewatia mbaroni washukiwa watatu zaidi wa ulanguzi wa mihadarati mjini Oyugis, kwenye msako unaoendelea dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya.
Washukiwa hao kati ya umri wa miaka 23 na 25 walinaswa baada ya kupatikana na misokoto 200 ya bangi.
Msako uliofanywa katika makao ya washukiwa hao ulifichua uozo zaidi baada ya kupatikana na mali inayoshukiwa kuwa ya wizi na pia silaha za kushiriki uhalifu zikiwemo rununu 11, vipakatalishi vitatu, pikipiki na gwanda la polisi.